20% NA MAN WALTER
Pia 20% aliiambai Enews kuwa tuzo tano zilipelekea watu wote kumuangalia yeye na hata wale waliokuwa wabaya wake hivyo mambo yalitokea mengi hali iliyopelekea yeye kushidwa kujikontroli na hatimaye likatokea bifu kubwa.
Hata hivyo 20% amesema tayari ameshamaliza bifu na Man Walter na hivyo watu watu wategemee mambo mazuri kutoka kwake na mziki mzuri kutoka kwake kwa maana yeye anavutu vingi ndani yake kwa hiyo mtegemee mengi tu kutoka kwake.
20% pia amewaomba radhi mashabiki zake kwa kipindi chote alichokaa kimya na kusema kuwa kwa sasa alisha gundua tatizo lililopelekea yeye kudondoka kimuziki na kusema kuwa kwa sasa amejipanga kuja kuchukua tuzo zaidi ya tano.








