Hayo yameweka wazi na taarifa rasmi iliyotolewa na Shirika hilo kupitia mtandao wake ambapo imesema itaendelea kufuatilia matokeo ya Sheria mpya iliyopitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hivi karibuni kwa kuzingatia makubalio na serikali ya ongezeko la asilimia 2 zilizokuwepo awali ambapo asilimia 1 ni kwa ajili ya usafirishaji kwenda nje.
Pia, taarifa hiyo imesema katika kipindi hiki kampuni ya ACACIA itaendelea kutimiza wajibu uliyowekwa kwa kuzingatia ongezeko la thamani uliyowekwa.



