Zarinah (Zari The Bosslady) kushoto akiwa na mama yake enzi za uhai wake.
Taarifa za kifo cha mama yake Zari zimethibitishwa na mrembo huyo kupitia ukurasa wake instagram.
"Tuna huzuni kubwa mimi na familia yangu kutangaza kifo chaa mama yangu kilichotokea leo asubuhi. Nafsi yake ipumzike kwa na Mwenyezi Mungu akusamehe dhambi zako" Baadhi ya maneno aliyoandika Zari.

Taarifa ya Zari kupitia Instagram
Pamoja na Taarifa ya zari bado hakuna taarifa maalumu iliyotoka kwenye familia ikiweka wazi ugonjwa uliokuwa ukimsumbua mama wa mrembo huyo.
Gazeti moja hapa nchini Alhamisi iliyopita liliripoti hali ya ugonjwa ya mama huyo kutokuwa nzuri baada ya kudaiwa kupumulia mashine ya oksijeni kwenye Kitengo cha Wagonjwa Mahututi (ICU) katika Hospitali ya Nakasero iliyopo nchini Uganda akisumbuliwa na maradhi ya moyo na figo ambayo yamekuwa yakimsumbua tangu kufariki kwa mkwe wake, Ivan Ssemwanga.
Bi. Halima alizaliwa Mei 15 1959 na amefariki Julai 20 2017. Tunawapa pole wafiwa na wote walioguswa na msiba huu. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi Amen.


