Monday , 13th Oct , 2014

Chama cha Wananchi CUF kimefanya mkutano wa kwanza visiwani Zanzibar toka Kupitishwa kwa Katiba inayopendekezwa kwa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania huku kikiweka msimamo wake wa kuikataa katiba hiyo.

Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Seif Sharif Hamad.

Akizungumza katika mkutano wa Hadhara uliofanyika katika uwanja wa Kibanda Maiti, Katibu Mkuu wa Chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad amesema Katiba hiyo imekikuka mkataba wa muungano ambao unataka Rais wa Zanzibar ndiyo awe makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Maalim Seif amesema kutokana na mapungufu hayo na mengine kadhaa, wamepanga kuikataa Katiba hiyo kwani haioneshi namna maslahi ya wananchi wa Zanzibar yatakavyokuwa ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Aidha Maalim Seif ameongeza kuwa Katiba ambayo wataikubali ni ile ambayo imezingatia maoni ya wananchi na imepata maridhiano kutoka pande zote mbili na yenye kukubalika kwa mujibu wa sheria.