Waziri wa Kazi na Ajira nchini Tanzania Gaudensia Kabaka
Akisoma bajeti ya makadirio ya wizara ya kazi na ajira leo Bungeni Mh. Gaudensia Kabaka amesema Programu hiyo inalenga kuwajengea vijana uwezo na ujuzi wa stadi mbalimbali wa kazi na ujasiriamali pamoja na kuwawezesha kupata mitaji nyezo na vifaa vya uzalishaji mali.
Aidha Mh. Kabaka amesema Program hiyo itawapatia vijana maeneo ya uzalishaji na biashara na kuongeza kuwa kwa mwaka 2014/2015 jumla ya ajira milioni moja laki tisa 29 elfu na mia tisa 38 ikiwa sawa na asilimia 200 ya lengo iliyowekwa na serikali.
Amesema kuwa ajira hizo zimezalishwa katika sekta ya umma, sekta ya kilimo, sekta ya elimu, sekta ya afya, sekta ya miundombinu, sekta ya nishati pamoja na miradi ya kijamii na nyingine serikali.
Mh. Kabaka ameongeza kuwa serikali imeandaa pia program maalum ya kukuza ujuzi wa nguvu kazi chini ya mpango wa matokeo makubwa sasa BRN, Wizara ya Kazi na Ajira kwa kushirikia na shirika la kazi duniani ILO, pamoja na wadau wengine katika kuboresha sekta ya ajira