Thursday , 4th Feb , 2016

Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi nchini Tanzania inaandaa sheria maalum itakayokuwa

Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi nchini Tanzania inaandaa sheria maalum itakayokuwa inawataka wamiliki wa nyumba wanaopangisha kwa bei kubwa kulipia kodi kama wanavyofanya wafanyabiashara wengine nchini Tanzania.

Akiongea na waandishi wa habari hii leo Jijini Dar esa Salaam Mkuu wa kitengo cha kodi katika Wizara hiyo Denis Rugemalila amesema kuwa kwa muda mrefu serikali ilikuwa imeliona suala hili lakini hakukuwa na sheria iliyoruhusu kuwabana wamiliki wa nyumba wanaofanya biashara hivyo wameamua kuandaa sheria itakayowapa mamlaka ya kukusanya mapato kutoka kwa wamiliki wa majengo.

Aidha, Wizara itawachukulia hatua ikiwa ni pamoja na faini wale wote walio badilisha matumizi ya ardhi bila ya vibali na kusababisha kero kubwa miongoni mwa jamaii ikiwemo ni pamoja na kujenga vituo vya mafuta au viwanda maeneo ya makazi ya watu hatua hizo ni pamoja na kulipishwa faini na kufikishwa mahakamani kwa wahusika.