Wednesday , 18th Jun , 2014

Robo tatu ya wanafunzi waliofaulu kidato cha nne kwa kupata daraja la kwanza hadi la tatu, wamechaguliwa kujiunga kidato cha tano.

Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI), Kassim Majaliwa.

Idadi hiyo ya wanafunzi watakaojiunga katika shule za serikali mwaka huu, imeongezeka kutoka 33,683 mwaka jana hadi kufikia 54,085 sawa na asilimia 75.6 ya wanafunzi 71,527 wenye sifa ya kujiunga na kidato cha tano Tanzania bara.

Akizungumza na waandishiwa habari, Naibu waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) Kassim Majaliwa amesema kati ya waliochaguliwa wanaume ni 31,352 na wasichana ni 22,733.