Friday , 11th Mar , 2016

Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera,Bunge ,Ajira na Walemavu,Jenister Mhagama ameitaka mifuko ya hifadhi ya jamii kuwekeza kwenye viwanda ili kuunga mkono msimamo wa serikali kuanzisha uchumi wa viwanda utakaotengeneza ajira na kuchochea maendeleo.

Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera,Bunge ,Ajira na Walemavu,Jenister Mhagama

Akizungumza katika Mkutano mkuu wa LPF unaoendelea jijini Arusha amesema mifuko hiyo ijikite zaidi katika uwekezaji ili kuweza kufikia malengo ya serikali ya awamu ya tano kuifanya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati.

Aidha Waziri huyo amesema kuwa Mifuko hiyo licha ya kuwekeza katika maeneo mbalimbali pia anapaswa kuangalia ni jinsi gani itakuza ajira katika uwekezaji huo ili kukabilinana na tatizo la Ajira linaloikabili Tanzania kwa sasa.

Mhagama ameitaka mifuko hiyo kuwekeza katika sekta ya viwanda kwa kuwa ndio Sekta inayotoa ajira kwa watu wengi zaidi nchini hivyo ni lazima wajitahidi kuisadia serikali katika kuinua uchumi kupitia sekta ya viwanda.