Chama cha Wastaafu na Wazee (CHAWAMU) mkoani Mtwara kimeitaka serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, kutatua changamoto zinazowakabili wazee ikiwa ni pamoja na kupitisha sera ya Taifa ya Wazee na kuwa sheria.
Akizungumza mkoani humo, katibu wa chama hicho, Wilberd Nandonde, amesema sera hiyo ambayo ilitungwa toka mwaka 2003 bado haijawa sheria na ni muda mrefu umepita jambo ambalo linasababisha changamoto nyingi zinazowakabili kuto fanyiwa kazi.
Miongoni mwa mambo ambayo anaamini yatatekelezwa iwapo sera hiyo itakuwa sheria, ni pamoja na huduma za matibabu bure kwa wazee ambapo ni changamoto inayolalamikiwa zaidi katika maeneo mengi hasa ya vijijini pamoja na halmashauri kuto toza kodi za majengo kwa wazee.
Kwa upande wake, mwanachama wa chama hicho, Blandina Geugeu, amesema matumaini ya wazee kwa sasa yamebaki kwa serikali hii ya awamu ya tano ambayo inaonekana kuanza kwa kasi katika kutetea masilahi ya wananchi na kwamba anaamini matatizo ya uhaba wa dawa katika hospitali za umma huku za madukani na hospitali binafsi zinapatikana litakwisha