Monday , 24th Nov , 2014

Upatikanaji wa chakula kwa wazee wasiojiweza katika kituo cha wazee cha Sarame wilayani Babati mkoani Manyara bado umelalamikiwa na wazee wa kituo hicho kuchangia kudhoofisha afya zao

Upatikanaji wa chakula kwa wazee wasiojiweza katika kituo cha wazee cha Sarame wilayani Babati mkoani Manyara bado umelalamikiwa na wazee wa kituo hicho kuchangia kudhoofisha afya zao na kufupisha siku za kuishi kutokana na serikali kudaiwa kuacha kupanga bajeti ya uhakika na kusababisha kusuasua kwa upatikanaji wa chakula hicho.

Wakizungumza katika kituo hicho wazee hao wamesema tangu mwezi Aprili mwaka huu wamekuwa wakikosa chakula cha uhakika ikiwa ni pamoja na kula mlo mmoja kwasiku,

Kwa upande wake mkuu wa kituo hicho Samsoni Munuo amekiri na kueleza bado hali ya chakula imekuwa tete kwani pamoja na kufuatilia hazina, wamekuwa wakiambiwa mtandao wa mawasiliano ni mbovu hatua ambayo inachangia mzabuni kuacha kusambaza chakula kutokana na serikali kuchelewesha malipo ya zabuni hiyo.

Kufuatia kusaasua huko, kikundi cha wanakwaya wa binti Sayuni cha KKKT Usharika wa Babati kimelazimika kupunguza makali ya njaa kwa kutoa chakula cha nafaka, maharagwe, mchele, matunda na miswaki, dawa za meno, viatu aina ya yeboyebo na vitu vingine kama sadaka kwao baada ya kuguswa kulingana na mazingira magumu ya wazee hao