Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa PBPA, Bw. Michael Mjinja
Katika utaratibu huo, sharti kampuni zinazoomba ziwe ni zile zilizosajiliwa na mamlaka za hapa nchini.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala hiyo Bw. Michael Mjinja, amesema kuanza kutumika kwa kanuni hizo kunalenga kuyapa uwezo makampuni ya ndani ambayo kwa mujibu wa kanuni na sheria za zamani yalikuwa hayana uwezo wa kushiriki katika zabuni hizo.
Bw. Mjinja ameongeza kuwa jumla ya kampuni tano zimeshiriki zabuni hiyo kati ya kampuni kumi na nane ambazo wakala amezipa vigezo vya kushiriki kuomba zabuni mbalimbali za uagizaji mafuta na kwamba nchi kwa sasa ina akiba ya kutosha ya mafuta yanayoweza kufika hadi mwezi Februari mwakani.




