Friday , 12th Feb , 2016

Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam kikosi cha kuzuia na kupambana na wezi wa magari kimewakamata watuhumiwa wawili kwa makosa ya kughushi nyaraka bandia za magari na leseni.

Akizungumzia hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Jeshi la Polisi Katika kukabilina na uhalifu wa aina mbalimbali, Kamada wa Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Saimon Siro amesema watuhumiwa hao walikamatwa maeneo ya Mburahati Barafu wakiwa na gari na baada ya kuwafanyia upekuzi walikutwa na vifaa mbalimbali vya kughushia nyaraka hizo.

Kwa upande mwingne Naibu Kamishna Siro amesema Jeshi hilo linawatafuta watuhumiwa wanne wanaodaiwa kufanya wizi katika mashine za kutolea fedha yaan ATM katika jiji la Dar es salaam.