Tuesday , 15th Mar , 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo amewaapisha wakuu wa mikoa wapya Ikulu jijini Dar es Salaam huku akiwataka kwenda kusimamia maendeleo ya wananchi pamoja na kutatua matatizo yanayowazunguka.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.

Akiongea na mbele ya wakuu hao wa mikoa na wageni waalikwa katka sherehe za kuwaapisha,Rais Dkt. Magufuli amewataka wakuu hao wa Mikoa wasisite kuwachukulia hatua watendaji wazembe ikiwa hata kuwaweka vituo vya Polisi kwa masaa 48 kwa kuwa sheria inaruhusu ili kuleta nidhani ya utendaji kazi.

Rais Magufuli ameongeza kuwa hatamvumilia Mkuu wa mkoa ambae atashindwa kutatua matatizo ya wananchi ikiwemo kushindwa kutatua migogoro ya ambayo inasabisha vifo vya mara kwa mara ikiwemo na kudhibiti Ujambazi katika mikoa yao.

Aidha Rais Magufuli amewetaka wakuu hao wa mikoa kuwasimamia Wakuu wa wilaya, Wakurugenzi na watendaji wengine ili kuleta mabadiliko ya kweli ingawa kuna baadhai ya watu wataathirika na hali hiyo lakini lazima Tanzania mpya yenye furaha kwa wote ipatikane.

Pia rais Magufuli amewataka wa kuu wa mikoa iliyo na rasimali za nchi kusimamia vizuri rasimali hizo vizuri iili kuleta maendeleo chanya huku akitolea mfano wa Mkoa wa Mtwara ambao zao la korosho limeonekana kuinufaisha hata nchi ya Vietnam wakati mkoa huo umebaki nyuma ikiwa ni pamoja na kushka kwa uzalishaji.