Thursday , 13th Aug , 2015

Watunga sera nchini wameshauriwa kuboresha mfumo utakaotoa fursa sawa kwa wananchi bila kujali kipato chao ili kuweza kupata huduma za kifedha kwa wafanya biashara wadogo,wa kati na wakubwa ili kuwapandishia kipato kulingana na matumizi husika.

Mkurugenzi mkuu wa mfuko wa kuendeleza sekta ya fedha Tanzania Sostenesi Kewe.

Hayo yamebainiswa na Mkurugenzi mkuu wa mfuko wa kuendeleza sekta ya fedha Tanzania Sostenes Kewe kwenye mafunzo kwa waandishi wa habari yanayolenga kufikisha ujumbe kwa watunga sera na kuboresha mfumo wa waandishi wa habari kuandika habari za kifedha kwa ufasaha zaidi pamoja na kuwasaidia wafanyabiashara wadogo kujua faida zinazo weza kupatkana katika matumizi ya huduma za ki fedha na kukuza mitaji yao.

Kwa upande wake mshauri wa mawasiliano wa mfuko wa kuendeleza sekta ya fedha Tanzania Neema Mosha amesema wataendelea kutoa mafunzo ya aina hiyo kila baada ya miezi sita ili kufikisha ujumbe wa matumizi ya fedha hadi vijijini

Waandishi wa habari walionufaika na mafunzo hayo wakisema yatawawezesha kuboresha uandishi wao kutokana na upeo watakaopata watakaopata.