Tuesday , 20th Feb , 2018

Jeshi la Syria limefanya mashambulizi makali dhidi ya eneo la Ghouta Mashariki linalodhibitiwa na waasi, ambapo inakadiriwa watu wasiopungua 98 wameuawa katika mashambulizi hayo yalianza usiku wa kuamkia leo, na taarifa zinadai hadi sasa yanaendelea

Picha hii haihusiani na tukio husika.

Kwa mujibu wa shirika la kuchunguza haki za binadamu nchini Syria lenye makao yake nchini Uingereza, limesema zaidi ya watu 100 wamekwishauawa katika mashambulizi hayo, wakiwemo watoto 20 na wanawake 15.

Umoja wa Mataifa umetoa wito wa kusimamisha mara moja kwa mapigano hayo.

Urusi ambayo ni mshirika muhimu zaidi wa serikali ya Syria, imekuwa ikijaribu kuanzisha juhudi za kidiplomasia kupunguza uhasama, na kupigia debe kuanzishwa kwa maeneo salama mnamo wakati huu mapigano yanapozidi kupamba moto.