Wanafunzi sita wa sekondari ya makatekista na mkuu wa sekondari hiyo Padri Hyasinti Kawonga wamefariki dunia na wengine26 kujeruhiwa kati ya hao wanne hali zao zikiwa mbaya baada ya ya gari aina ya Land Rover One-Ten kutumbukia kwenye korongo na kuwaka moto katika kata ya Kigonsera wilayani Mbinga mkoani Ruvuma.
EATV imefika eneo la tukio Kigonsera wilayani Mbinga mkoa wa Ruvuma na kushuhudia kijiji cha Kigonsera kikiwa katika hali ya simanzi ambapo mganga mfawidhi wa kituo cha afya Kigonsera Dkt Patrick Mhagama amesema wamepokea miili saba na majeruhi ishirini na sita.
Dkt. Patrick pia amesema kwamba miili imeungua vibaya kiasi cha kushindwa kutambulika baada ya gari hilo kuwaka moto .
Mashuhuda wa tukio hilo wanasema ajali hiyo ilitokea baada ya kufeli breki na dereva ambaye alikuwa marehemu Padri Hyasinti Kawonga akakata kona ndipo alipoingia kwenye korongo na ikatokea shoti na gali likawaka moto.
Hilo ni tukio la tatu katika miaka tofauti kuua watu saba ambapo kuna wanajeshi saba walikufa kwa ajali ya gari na kufuatiwa na ajali ya maji ilioyoua watoto saba waliosombwa na maji katika kata ya Kigonsera..
Mwenyekiti wa kitongoji cha Misheni katika kata ya Kigonsera bw. John Kafarapia amesema ni pigo kufiwa na padri Kawonga aliyekuwa mkuu wa shule ya sekondari ya makatekista na mfadhiri wa wananchi mbalimbali.