Friday , 24th Jun , 2016

Waziri wa nchi,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,(TAMISEMI), Mhe. George Simbachawene, amesema kuwa serikali imetenga shilingi bilioni 16 kwa ajili ya kuhudumia shule zenye watoto wenye ulemavu nchini.

Waziri wa nchi,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,(TAMISEMI), Mhe. George Simbachawene.

Akizungumza jana Bungeni Mjini Dodoma katika kipindi cha maswali na majibu, Mhe. Simbachawene amesema kuwa serikali katika mpango wake wa utoaji elimu bure kuanzia shule ya msingi hadi kidato cha nne umelenga watoto wote nchini.

Mhe. Simbachawene amesema kuwa kuhusu watoto wenye ulemeavu ambao wanachaguliwa kujiunga na kidato cha tano suala hilo lipo chini ya wakuu wa wilaya ambao wamepewa miongozo ya kulishughulikia.

Aidha, Waziri huyo wa TAMISEMI, ametumia fursa hiyo bungeni kuwataka wazazi na walezi nchini kuhakikisha wanawapelekea watoto hao shule ili wapate haki ya elimu kwa serikali imeshatenga fungu kwa ajili ya kuwahudumia.

Katika swali la msingi la Mbunge wa viti Maalum(CHADEMA),Dkt. Elly Macha, Simbachawene amesema Mamlaka za serikali za Mitaa zimekuwa zikiingia kati kwa kutoa misaada ya watoto wenye mahitaji maalumu pale panapojitokeza.

Sauti ya Waziri wa nchi,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,(TAMISEMI), Mhe. George Simbachawene,