Friday , 23rd May , 2014

Kikundi cha wahalifu kinachojiita Panya Road ambacho zamani kilikuwa kikijiita Watoto wa Mbwa chenye maskani yake Ilala jijini Dar es Salaam, kimelalamikiwa na wakazi wa maeneo hayo kwa kuendesha vitendo vya uporaji na kujeruhi.

Mkuu wa polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna wa Polisi Suleiman Kova.

Wakizungumza na East Africa Radio huku wakiwa na hali ya wasiwasi baadhi ya wakazi wa maeneo ya Ilala na Buguruni wamesema kikundi hicho kimekuwa kikifanya vurugu katika sehemu tofauti na kuwalamisha watu kutoa mali au pesa alizonazo na kuwatishia huku wakiwa na silaha tofauti.

Katika moja ya tukio wakazi hao jana wamelazimika kukimbia hovyo mara baada ya kuwepo kwa taarifa za kikundi hicho kuvamia maeneo ya Buguruni Malapa kwa lengo la kujeruhi watu na kuwapora mali zao.