Tuesday , 1st Dec , 2015

Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Glorious Luoga, amewaagiza maofisa wanaotoa vibali vya kusafirisha au kuingiza mahindi nchini katika mpaka wa Silali waache mara moja tabia ya ukiritimba kuwahangaisha wafanyabiashara wa mahindi.

Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Glorious Luoga

Mkuu huyo wa wilaya hiyo ametoa agizo hilo wakati wa mkutano na watendaji wa mpaka wa silali na wafabiashara wa mahindi na kuongeza kuwa baada ya kikao hicho hataki kusikia ukiritimba huo unaendelea.

Hatua hiyo inakuja baada ya malalamiko ya wafabiashara kudai kuwa kuna baadhi ya watendaji wanawahangaisha wafanyabishara hao katika kutoa vibali na kupelekea usumbufu wa kuvusha au kuingiza bidhaa zao nchini.

Luoga amesisitiza watendaji watafute utaratibu mzuri ambao utaweza kuwapa urahisi wafanyabiashara wa pande zote mbili urahisi wa kufanya biashara zao ikiwemo na kuacha kutengeneza mazingira ya kutaka kupewa rushwa.