Monday , 15th Dec , 2014

Serikali imekiri mapungufu katika Uchaguzi wa Serikali Mitaa uliofanyika jana, na kusema itawachukulia hatua watendaji wake watakaobainika kufanya uzembe na hata kama ni yeye asema yuko tayari kuwajibika.

Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),

Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), nchini Tanzania Mh. Hawa Ghasia amesema serikali itawawajibisha watendaji wote wa serikali waliohusika na kuvurugika kwa uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika nchini kote hapo jana.

Akitoa ripoti ya awali ya tathmini ya uchaguzi wa serikali za mitaa Mh. Ghasia amesema kwa sasa wanafanya uchunguzi ili kubaini watendaji hao na kuongeza kuwa hata yeye akiwa waziri na msimamizi mkuu wa uchaguzi huo ikibainika alihusika kuvuruga uchaguzi huo atawajibika.

Katika tathimini hiyo ya awali ya uchaguzi wa serikali za mitaa Mh. Ghasia pia amemtaja mpiga chapa mkuu wa serikali ambae alihusika kuchapisha karatasi za kupigia kura katika baadhi ya maeneo kuchapisha karatasi hizo kimakosa na kurejeshwa kwa ajili ya kuzifanyia marekebisho lakini makosa yalionekana kujirudia tena.