Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohamed Shein.
Dr. Shein ametoa tahadhari hiyo visiwani humo wakati akiufunga mkutano wa Nane wa baraza la biashara la Zanzibar ambapo amesema ni jambo la kushangaza kuona baadhi ya watendaji wamekuwa wakijali maslahi yao na kuidharau serikali na kuongeza kuwa serikali imepania kuleta mabadiliko ya uchumi kwa kushirikiana na sekta binafsi..
Mapema Balozi Seif Ali Idi, Makamu wa pili wa Rais ambaye ndiye Mtendaji Mkuu wa serikali amekiri kuwepo kwa urasimu wa watendaji katika kupitisha miradi ya uwekezaji hali ambayo inaiharibia jina Zanzibar ambapo baadhi ya taarifa zinazosambazwa zinaitangaza vibaya Zanzibar juu ya uwekezaji.
Hata hivyo waziri wa biashara,viwanda na masoko Mhe Nassor Ahmed Mazrui akitoa tathmini ya biashara amesema pamekuwepo na ongezeko kubwa la biasharaza nje na kwa upande wa bishara ya ndani pande mbili za muungano zimepata mafanikio makubwa ya biashara.
Mkutano huo wa Nane ambao Mwenyekiti wake ni Rais wa Zanzibar unawakutanisha watendaji wote wa serikali na wafanyabishara wa sekta binafsi.