Friday , 17th Jul , 2015

Watanzania wametakiwa kuzingatia mila na desturi zilizopo katika familia zao zilizokuwa zikienziwa na vizazi vilivyopita kuepuka laana na mikosi kunako pelekea majanga kushamiri ikiwemo ajali na magonjwa yasiyotibika

Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili wa MUJATA, Chifu Shadrack Merere.

Ushauri huo umetolewa na viongozi asasi ya muungano wa jamii Tanzania MUJATA wakiwa katika moaja ya pori la kudumisha mila kijijini chaloe wakati wakimsimika rasmi bibi mkuu anayedumisha mila na desturi Bi. Germana Livifile mkazi wa kijiji cha igwachanya wilayani wangingo'mbe mkoani njombe

Mshauri wa asasi ya MUJATA hapa nchini Peter kayemba amesema kuwa kufuatia jamii kukosa mwelekeo dhini ya imani ya kweli wamelazimika kuwatambua wazee wa kimila katika mikoa mbalimbali hapa nchini ili kulinda haki ya mtu kuabudu

Akizungumza mbele ya viongozi wa asasi ya mujata pamoja na na mashuhuda waliowahi kutambika na kufanikiwa akiwa katika msitu huo wa magoda chaloe unaotumika kwa matambiko ya asili.

Bi. Germana Livifile amesema pamoja na kutoa huduma ya kuikomboa jamii lakini madhehebu ya dini za kikristu kijijini hapo yamekuwa yakimpiga vita kwa kuuchoma moto

Pia amesema kuwa majanga yanayo likumba taifa zikiwemo ajali za magari pamoja vifo visivyo vya lazima vinatokana na kupuuzwa kwa mila na desturi za kale.

Baadhi ya mashuuda walowahi kupata huduma kutekeleza mila za asili kuondokana na mikosi wameishauri serikali kuona namna ya kuwahifandhi wazee wa kale wanaodumisha mila kwa kuwaendeleza na kuwalinda dhidi ya watu wabaya kama anavyoeleza Lugazia Kamugisha kutoka mkoani Kagera

Mika Amoni Kanyatuka mkazi wa mkoa Mbeya alikuyekuwa anakumbwa na matatizo ya kupotelewa fedha pamoja na maradhi mfululizo anakiri kupata huduma na kueleza kuwa hali sasa ni shwari katika familia yake

Nyumbani kwa bibi Germana kijiji cha Igwachanyanya ndiko kunafanyika utambuzi wa matatizo kabla ya kufika katika msitu wa mila na desturi na kuna wagonjwa wengi wanasubiri huduma Neno komba ni miongoni mwa wagonjwa wa kichaa lakini baada ya kufika kwa bi germana amepata nafuu.