Friday , 31st Jul , 2015

Wananchi wanaoishi katika maenao ya mpaka kati ya Tanzania na Burundi katika mkoa wa kigoma , wametakiwa kuwafichua raia wa nchi jirani wanaoingia kinyemela na kuingiza silaha mbalimbali za kivita nchini.

Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru mwaka 2015 Bw.Juma Khatibu Chum akiongea na wananchi

Wito huo umetolewa na kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru mwaka huu Juma Khatib Chum wakati akizungumza na wananchi katika kijiji cha Mnanila wilayani Buhigwe baada ya Mwenge kukimbizwa katika wilaya hiyo na kuzindua miradi mbalimbali ya maeneleo yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni moja nukta moja

Amesema ni lazima wananchi wanaoishi mpakani wawe makini licha ya kwamba tuna jukumu la kuwapokea na kuwahifadhi kama wakimbizi raia wa burundi wanaoikimbia nchi yao .

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Buhigwe Mary Tesha amesema pamoja na changamoto kadhaa zinazoikabili wilaya hiyo mpya, wameanza kujenga miundombinu ya barabara na nyumba za watumishi pamoja na kupima viwanja ili kuujenga mji wa makao makuu ya wilaya hiyo