
ili kupata viongozi bora watakaowachagua kwa sifa zao na si kwa ushawishi wa rushwa.
Wito huo umetolewa na Kamanda wa TAKUKURU mkoani Morogoro Emanuel Kiabo,alipokuwa akiongea na East Africa Radio, alipokuwa akitoa elimu maalum na maafisa wengine wa TAKUKURU katika maeneo ya masoko na vituo vya mabasi, wakiwa na lengo la kuwafikia vijana walio nje ya mfumo rasmi wa elimu.
"Wito wangu kwa wanannchi ni kwamba tutambue ya kwamba kipindi cha uchaguzi, ni kipindi cha kuchagua viongozi wanaostahili kuongoza kwa kipindi cha miaka mitano, wananchi wasikubali kupewa kitu chochote kidogo mno, kwa sababu hata wakipewa kiasi gani cha fedha hakiwezi kuwa sawa na thamani ya miaka mitano mtu anapoingia madarakani", Alisema Emanuel.
Emanuel alisema kwamba wameamua kuchukua hatua hiyo ya kuingia kwenye maeneo hayo kwani kuna vijana wengi ambao hawako kwenye mfumo rasmi wa elimu, hivyo wanakosa elimu muhimu dhidi ya rushwa kwa kipindi hiki cha uchaguzi, hivyo wanaamini wakielimishwa vya kutosha vitendo vya rushwa vitapungua.
"Tumeona kwamba ipo haja ya kuwafikia vijana ambao wako nje ya mfumo rasmi wa elimu, na maeneo haya ni maeneo ambayo yana mkusanyiko wa vijana, kwa mfano maeneo ya stand, maeneo ya masoko, na mada yetu kubwa ni wajibu au nafasi ya vijana na mapambano dhidi ya rushwa hususan kipindi hiki kulekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, tunaamini vijana wakielimishwa vizuri, wakakemea vitendo vya rushwa, rushwa itapungua kwa kiasi kikubwa sana, na hivyo kupata viongozi walio bora", alisema Emmanuel.
Nae Afisa TAKUKURU kutoka makao makuu Bi. Dorothea Mrema, amesema wana mkakati wa kuelimisha vijana wajibu wao katika mapambano dhidi ya rushwa katika uchaguzi mkuu, wakiwa na lengo la kuhakikisha vijana wanachagua viongozi bora na wasio jihusisha na rushwa, kwani vijana ndio chachu ya mabadiliko katika jamii yoyote.