Friday , 10th Jun , 2016

Rais wa Ufaransa, Francois Hollande, ameonya dhidi ya jaribio lolote la kutibua ufunguzi wa michuano ya Euro 2016 leo.

Rais wa Ufaransa, Francois Hollande.

Rais wa Ufaransa, Francois Hollande, ameonya dhidi ya jaribio lolote la kutibua michuano ya Euro 2016 kwa mgomo, katika kuelekea ufunguzi wa michuano hiyo mikubwa ya soka Barani Ulaya hii leo.

Nchi ya Ufaransa imetumbukia katika mgogoro na wafanyakazi, uliochochewa na mabadiliko sheria za ajira, na mgomo wa wahudumu wa treni hii leo unaweza kuathiri ufunguzi wa michuano hiyo.

Madereva wa treni za abiria wametishia kugoma leo kutoa huduma katia njia ya kuelekea kwenye uwanja wa mpira wa Stade de France huko St Denis nje ya Jiji la Paris, ambako ndipo mchezo wa France na Romania utafanyika.