
Hayo yameelezwa jijini Dar es salaam na Mratibu wa chama cha wasioona mkoa wa Dar es Salaam Bw. Ally Abdallah wakati wa mahojiano na East Africa Rado kuhusu hali ya huduma mbalimbali na uelewa wa jamii kuhusu watu wenye ulemavu wa kuona.
Aidha mratibu huyo ameeleza kuwepo kwa changamoto ya kunyanyapaliwa katika nafasi za ajira kwa imani kwamba watu wenye ulemavu wa kuona hawana uwezo jambo ambalo halikufanyiwa tafiti za kutosha na watu hao kuendelea kukosa ajira.