Tuesday , 3rd May , 2016

Baadhi ya wapagazi Mkoani Kilimanjaro wamelalamikia tabia ya uongozi wa watalii ya kuomba rushwa ya Ngono,ili kuwapatika kazi za kuwapandisha watalii katika hifadhi ya Mlima Kilimanjaro.

Mhifadhi katika Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro,KINAPA ,Charles Ngendo akiwatambulisha wageni kutoka Afrika Kusini

Wakizungumza walayani Moshi wakati wa mafunzo kuhusu Ugonjwa wa Ukimwi,wapagazi hao wamesema kuwa wanalazimika kukubali rushwa hiyo hasa kwa wapagazi wanawake kutokana na hali ngumu ya maisha.

Wakiwa katika mafunzo hayo ambayo yameshirikisha takribani wapagazi 50 ambao kazi yao ni kubebea mizigo wakati wote watalii wakiwa mlima kilimanjaro wamesema kuwa changamoto hiyo ya rushwa ya ngono ndio sababu kubwa ya kusambaa kwa virusi vya Ukimwi.

Mhifadhi wa utalii katika hifadhi ya taifa ya mlima Kilimanjaro, Charles Ngendo, amesema wapagazi ni watu muhimu katika sekta ya utalii hivyo wanapasawa kupewa elimu ya kujifunza madhara ya ugonjwa wa Ukimwi mara kwa mara.

Akizungumza na Waandishi Katibu wa Chama cha Waongoza watalii,Mkoani Kilimanjaro, James Mong'ateko, amesema suala hilo lipo na kwamba ameomba uongozi wa hifadhi ya Mlima huo kuwaandalia utaratibu wa malazi wapagazi wanawake.