Mratibu Mkuu wa Umoja wa Waganga na Wakunga wa Tiba Asili Tanzania (Uwawata), Julius Juju (wapili kulia) akiwa na viongozi wengine wakimkabidhi Waziri wa Mambo ya Ndani ripoti yao
Imeelezwa kuwa licha ya juhudi zinazofanywa katika kukomesha mauaji hayo viongozi na wanasiasa wamekuwa ni mstari wa mbele kuwatetea watuhumiwa wa vitendo hivyo hatua ambayo inasababisha uendeshaji wa kesi kuwa mgumu.
Wakiongea baada ya kutembelea Shule ya Msingi Mitindo iliyopo wilayani Misungwi mkoani Mwanza Umoja huo umesema licha ya Changamto hiyo wanayokutana nayo lakini bado wanafanya juhudi za kupambana na hali hiyo kutokana na wengi wao kudaiwa kuhusika na suala hilo.
Shule ya Msingi Mitindo, Wilayani Misungwi Mkaoni Mwanza ina jumla ya wanafunzi 213, kati yao wenye ulemavu wa ngozi ni 87 idadi ambayo ni kubwa kuliko wanafunzi wenye mahitaji mengine.





