Thursday , 27th Aug , 2015

Zaidi ya shilingi bilioni 2.3 zimeanza kugawiwa kwa wananchi kama ruzuku kwa kaya masikini mkoani mbeya kupitia mpango wa TASAF awamu ya tatu ambao unalenga kunusuru kaya masikini nchini.

Mkuu wa mkoa Mbeya,Abasi Kandoro

Zoezi la utoaji wa ruzuku hiyo mkoani mbeya limezinduliwa wilayani kyela na mkuu wa mkoa wa mbeya, Abbas Kandoro ambaye amewataka wananchi kuacha tamaa ya kutumia fedha hizo kwa mambo ya hovyo na badala yake akasisitiza zitumike kusomesha watoto, kuwezesha upatikanaji wa huduma za afya kwa wanakaya na shughuli za uzalishaji.

Mratibu wa TASAF mkoa wa Mbeya, Aika Temu amesema kuwa ruzuku hiyo ni fursa pekee kwa kaya masikini mkoani Mbeya kujikwamua na umaskini.

Baadhi ya walengwa wa mpango huo wamesema kuwa fedha hizo zitawasaidia kupunguza makali ya maisha kutokana na sasa kukabiliwa na changamoto ya kusomesha watoto.