Friday , 9th Nov , 2018

Wananchi wa kijiji cha Minjingu wilayani Babati Mkoani Manyara wamesusia zaidi ya shilingi milioni 300, zilizokuwa zinapatikana kwenye mapato yatokanayo na eneo la hifadhi iliyopo kwenye kijiji chao kutokana na serikali kuwafukuza kwenye maeneo yao ya malisho yaliyopo kwenye hifadhi ikiwa

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti.

ni sehemu yao ya kambi ya kulisha mifugo.

Miongoni mwa sababu zilizotajwa na wanakijiji hao kususia milioni hizo miatatu ni kwa kile kilichodaiwa kuwa wao ni wamiliki halali wa eneo hilo la hifadhi ambapo walihitaji kupata fedha hizo bila ya kuwepo kwa mgao wa serikali.

Aidha wananchi hao wamelalamikia serikali kutowapatia fidia za uharibufu uliofanywa na wanyama katika mazao yao na kuwapa sababu ya kuhoji kwanini serikali iwape asilimia 50 ya wakati hawahusiki kwenye ulipaji wa gharama za uharibifu wa mazao yao.

Akizungumza na wanakijiji hao Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti amesema kwa sababu kijiji hicho kipo katikati ya hifadhi ya tarangire na hifahi ya Burunge wanakijiji watalazimika kuhama kama hawataklubaliana na maagizo ya srikali.

"Nawapa masaa 3 mpaka kesho hizo hela muwe mshazitoa kwenye akaunti yenu milioni 300, toa hela zote peleka kwenye kituo cha afya si hawazitaki watu wamekataa hela kwanini unawalazimisha peleka zote kujenga kituo cha afya," amesema Mnyeti