Mbunge wa Vunjo akiwa na wananchi wa jimbo hilo
Wananchi wa jimbo la Vunjo wilayani Moshi wafanya maandamano makubwa kuishinikiza serikali iwatendee haki katika ugawaji wa ardhi ekari la 2000 za shamba la ushirika la Lokolova ambalo serikali mkoani Kilimanjaro imelichukua bila ridhaa ya wanaushirika kwa ajili ya ujenzi wa soko la kimataifa..
Mbunge wa vunjo Mh. Augustine Mrema amesema, ingawa wananchi wa jimbo hilo hawana tabia ya kufanya vurugu lakini katika suala la ardhi hiyo yeye ataongoza maandamano hayo ili kuhakikisha wananchi wanaingia mkataba katika umiliki wa ardhi hiyo kama walivyofanya wananchi wa kigamboni.
Mh Mrema amesema hayo alipoongea na wananchi wa kata za jimbo hilo katika mji mdogo wa Himo kuwaeleza hatua mbalimbali anazochukua kurudisha mikononi mwao ardhi ya mieresini, Lokolova na Kilemapofo.