
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dodoma, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais –Tamisemi, Selemani Jafo amesema kati ya wanafunzi hao, wasichana ni 31,884 na wavulana 39,020.
"Wanafunzi waliochaguliwa ni kati ya 92,712 wa shule na taasisi ya elimu ya watu wazima waliokuwa na sifa za kuchaguliwa kujiunga na kidato cha tano, vyuo vya ufundi na vyuo elimu ya kati", amesema Jafo.
Aidha, Waziri Jafo amesema utaratibu uliozingatiwa wa kuwachagua wanafunzi hao ni kuangalia alama za ufaulu wa daraja, daraja la ufaulu, ufaulu katika masomo ya sayansi, jinsia na nafasi zilizopo kwenye kozi na vyuo husika.