Rais wa serikali ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo(SUA), Osca Ndunguru
Akizungumza na waandishi wa habari chuoni hapo Rais wa serikali ya wanafunzi wa chuo hicho Oscar Ndunguru ametupia lawama bodi ya mikopo kuendelea kuwatesa wanafunzi licha ya serikali ya wanafunzi kuwasilisha vielelezo hivyo hali inayosababisha wanafunzi hao kuishi kwa tabu chuoni.
Aidha wanafunzi hao wamemuomba Rais Magufuli kutembelea bodi ya mikopo kuchunguza uozo unaofanyika na kwamba bodi hiyo ihakikishe inashugulikia tatizo la wanafunzi hao ndani ya siku tatu.
Nao baadhi ya wanafunzi walioathiriwa na tatizo la kukosa mikopo wameeleza kusikitishwa kwao na kwamba wanalazimika kuishi kwa tabu kwa kukopeshana wanafunzi kwa wanafunzi wakitegemea bodi ya mikopo itawalipa fedha zao lakini kadri siku zinavyozidi kusonga mbele hali ya maisha yao chuoni yanazidi kuwa magumu
Waziri mkuu wa serikali hiyo ya wanafunzi amesisitiza na kuiomba serikali ya Rais Magufuli kuangalia upya mfumo wa utendaji wa watumishi wa bodi ya mikopo kwani wanafanya kazi hiyo kwa mazoea na upendeleo kwa baadhi ya watu hali inayozorotesha maendeleo ya nchi.