
Ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania ATCL.
Kwa mujibu wa Mbunge Masoud Salim, watu hao ambao walitajwa kwenye ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali CAG, inasemekana waliingizia taifa zaidi ya hasara ya shilingi bilioni 92.
"Mkaguzi wa serikali alisema hatua za kinidhamu zichukuliwe kwa wale wote ambao walilingiza Shirika la Ndege la Taifa kwa hasara ya bilioni 92 ambao waliingia mikata mibovu kwa kununua ndege ambayo ilikua mbovu. Je lini serikali itasikiliza ushauri wa CAG"
Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye amesema Serikali imeunda tume kuchunguza suala hilo kwa ajili ya kupata ukweli ili iweze kuwachukulia hatua za kisheria.
"Tumeunda tume, maalum ya kushughulikia suala hilo na mbunge atulie tutajua ukweli muda si mrefu. " alijibu Naibu waziri
Awali mbunge huyo aliuliza juu ya lini ambapo serikali ya Tanzania itailipa mamlaka ya viwanja vya Zanzibar inayoidai Shirika la Ndege la Taifa
zaidi ya shilingi milioni 200 ambapo serikali inamalizia kufanya upembuzi ili kujua deni halisi