Tuesday , 19th Apr , 2016

Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Hassan Suluhu, amewaagiza wakuu wa mikoa nchini kutenga maeneo ya wajasiriamali kufanya biashara zao kwa siku za jumapili ili kujiongezea kipato.

Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Hassan Suluhu,

Mhe. Suluhu ametoa kauli hiyo jana Mkoani Morogoro wakati wa Sherehe za kuwasha Mwenge wa Uhuru ambapo amesema kuwa wakuu wa mikoa waweke pia mazingira wezesheji ya ufanyaji biashara kwa wajasiliamali hao kwa kila mkoa nchini.

Aidha Makamu wa rais amewataka wakuu hao wa mikoa kuhakikisha kuwa katika siku hizo wajasiriamali hao walipe ada zinazostahiki katika eneo lile,na kutunza mazingira ya maeneo wanayopewa na kuweka ulinzi wa kutosha katika maeneo yao ya biashara na wawajibike ipasavyo.

Aidha Mhe. Suluhu ameongeza kuwa serikali itatenga maeneo rasmi ya shughuli za vijana na kuwawezesha vijana kupata mitaji na nyenzo za kufanyia shughuli zao za kiuchumi na huduma kwa jamii.