Thursday , 28th Apr , 2016

Wakuu wa idara wa Halmashauri zote Mkoani hapa wametakiwa kwenda na kasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Magufuli, katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku ya kuwatumikia wananchi na kuwaletea maendeleo wanayohitaji.

Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Halima Dendego,

Akizungumza katika uzinduzi wa mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3), Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendego, amewaeleza viongozi hao kuwa wakati huu ni wa kufanya kazi, na wenye tabia za kuzembea wanapaswa kujifunza kutokana na yanayowakuta viongozi wengine wenye tabia hizo.

Aidha, amesemam ujio wa mradi huo utasaidia kwa kiasi kikubwa kuboresha masuala ya utawala bora ikiwa ni pamoja na kuimarisha mifumo ya mawasiliano, fedha na utendaji ambapo utaifanya jamii kutambua mambo mbalimbali yanayofanywa na viongozi wao.

Mtaalamu wa fedha wa mradi huo Abdul Kitula, akizungumza kwa niaba ya mkurugenzi mkuu wa mradi, amesema halmashauri kupitia mradi huo wenye thamani ya dola za Kimarekani Milioni 62, zitanufaika kwa kuimarika mifumo yao katika utawala bora, fedha, rasilimali watu pamoja na mifumo ya utendaji tafiti.

Sauti ya Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Halima Dendego,