Thursday , 30th Apr , 2015

Wakurugenzi wa Manispaa Nchini wametakiwa kuanzisha Ushirika wa wananchi kwa ajili ya kupanga miji yao wenyewe kwa ajili ya kuboresha miji na majiji kwa haraka hapa nchini.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI Bw. Jumanne Sagini.

Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu wa TAMISEMI, Edwin Kiliba wakati akiongea na makatibu tarafa na wakurugenzi 19 waliokwenda nchini Japan kwa ajili ya mafunzo ya maboresho kwa watendaji wake kwa mikoa minne ya Dar esalaam, Mtwara, Lindi na mji wa Tunduma.

Amesema kuwa ni lazima sasa watanzania waige kwa waliofanikiwa katika kupanga miji yao kama nchi ya Japan ambapo wananchi wake huungana katika ushirika na kupanga miji yao kwa kujenga barabara, Zahanati, kufanya usafi, na kuanzisha miradi mbalimbali ya maendeleo.

Kiliba pia amewataka Watendaji hao kuhakikisha halmashauri zao zinakusanya kodi kwani Japan halmshauri hukusanya kodi kwa 67% na hutegemea 33% toka serikali kuu wakati hapa Nchini halmashauri hupata 95% ya bajeti yao toka Serikali kuu,