Friday , 14th Jun , 2019

Wakulima wa zao la muhogo kutoka Wilaya za Kakonko, Kibondo na Kasulu mkoani Kigoma, wameiomba Serikali iwasaidie namna ya kupata soko la zao la muhogo kwa kile walichokieleza kwa sasa wanauza zao hilo kwa hasara.

Wakulima hao wametoa malalamiko hayo mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Kibondo Luis Bura, kuwa kinachowafanya kwa sasa kuuza zao hilo kwa hasara ni uwepo wa madalali, wanaojipangia bei.

Akizungumzia kero hiyo Mkuu wa Wilaya ya Kibondo Luis Bura amesema kuwa "kwa sasa hatuwezi kuamua lolote, niwaombe wakulima mtuite wote kwa pamoja kutoka Wilaya ya tatu, ili kutatua changamoto hii kama Wanakibondo ili tuwe na sheria ya pamoja na ndugu zetu wa Kakonko, na kusulu"

Mwishoni mwa mwaka jana Wakulima wa zao la korosho nchini, waliingia kwenye mgogoro wa bei ya bidhaa hiyo kufuatia kutokukubaliana na wafanyabiashara ambapo Wakulima waligoma kuuza zao hilo kwa bei ya hasara, mpaka Serikali iliopingilia kati.