Friday , 19th Jun , 2015

Zoezi la kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura mkoani Kagera linaendelea kusuasua ambapo leo ni siku ya sita wananchi wanalala usikukucha katika vituo vya kujiandikisha wakiwa wamepanga foleni bila mafanikio.

Baadhi ya wanchi wakiwa katika kituo cha kujiandikisha

Zoezi la kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura mkoani Kagera linaendelea kusuasua ambapo leo ni siku ya sita wananchi wanalala usikukucha katika vituo vya kujiandikisha wakiwa wamepanga foleni bila mafanikio.

EATV imefika katika vituo vya kuandikishia mapema leo asubuhi na kushuhudia watu wakiwa wamelala usiku kucha katika kituo cha Matopeni, kasha na Nyangoe ambapo wananchi wamesema wamekuwa wakifanya hivyo kwaajili ya kuwahi foleni asubuhi huku wakiwatupia lawama waandikishaji kwamba wameendekeza rushwa kwa kuwapitisha watu wenye pesa hukuwa wao wakiendelea kubaki bila kujiandikisha hali ambayo imewaathiri kwa kiasi kikubwa.

Baadhi ya wazee na akinamama wajawazito na wenye watoto wachanga wamesema hali hiyo imewaaathiri kiuchumi kwani siku zote hizo wameahirisha shughuli mbalimbali na kushinda katika vituo vya kujiandikisha huku wakinyeshewa na mvua na kwamba mpaka sasa hawajafanikiwa kujiandikisha ambapo wameiomba tume ya taifa ya uchaguzi kuongeza muda wa kujiandikisha.

Akiongea na EATV afisa uchaguzi wa manispaa ya Bukoba Erick Bazampola amesema pamoja na changamoto zinazowakabili katika zoezi hilo lakini mpaka sasa wamefanikiwa kuandikisha watu 59,000 sawa na asilimia 65 na kwamba watu bado ni wengi lakini pia ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi ili waweze kuandikishwa kwani zoezi hilo linatarajia kukamilika siku ya kesho.

Tags: