
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makala
Akiwa katika ziara yake wilayani Mbeya, Naibu Waziri huyo amefika katika kijiji hicho ambako mradi wa maji unaosimamiwa na halmashauri unasuasua, na ndipo akina mama wa kijiji hicho ambao walimueleza kadhia wanayoipata.
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Mbeya, Anderson Kabenga maarufu kwa jina la ndombolo ya solo, amesema kusuasua kwa mradi wa maji wa iwindi kunatokana na mkandarasi aliyepewa kazi hiyo kusimamishwa baada ya kubainika kuwa hana uwezo, lakini pia akadai kuwa halmashauri yake licha ya kuendelea na mchakato wa kumpata mkandarasi mwingine pia haina fedha za kutosha kukamilisha mradi
Baada ya kuwasikliza wananchi hao, Naibu Waziri wa Maji, Amos Makala akalazimika kuwatuliza kwa kusema kuwa kuanzia sasa suala hilo linachukuliwa kwa uzito mkubwa na serikali, huku akiahidi kwamba wakati wowote kuanzia sasa halmashauri ya wilaya ya mbeya itapokea shilingi milioni 195 zitakazoelekezwa kwenye mradi huo na kwamba atakapofika wizarani atahakikisha fedha zaidi zinaletwa kwa ajili ya ujenzi wa mradi huo.
Mradi wa maji wa iwindi ambao kwa sasa unasuasua, ujenzi wake unahitaji fedha zaidi ya shilingi bilioni moja na utakapokukamilika utasaidia wananchi zaidi ya 6000 katika vijiji vitatu vya kata ya iwindi kupata maji safi na salama.