Friday , 26th Jun , 2015

Wakazi wa mji mdogo wa Ilula wilaya ya Kilolo wameiomba serikali kuwapatia huduma ya maji ili kuondokana na usumbufu wa kusafiri umbali wa kufuata huduma hiyo.

Mbunge wa jimbo la Kilolo Prof. Peter Msola akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mwatasi katika kata ya Bomalang'ombe katika jimbo la Kilolo.

Wakizungumza na East Africa Radio wamesema wanapata huduma ya maji ya bomba mara moja kwa wiki hali inayopelekwa kutotoshereza mahitaji ya kila siku huku wanafunzi wakitumia mda mwingi kutafuta huduma hiyo hali inayopelekea kukosa muda wa kujisomea.

Kwa upande wa Bw. Ahazi Challi ambaye ametangaza nia ya kugombea ubunge jimbo la Kilolo kupitia CHADEMA ameahidi kuitumia mito ya ruaha,lukosi na mgombezi ili wananchi waweze kuondokana adha hiyo.

Aidha, Bw. Challi ameongeza kuwa atahakikisha anaboresha miundo mbinu ya barabara na mawasiliano, matibabu na dawa, elimu,kilimo na uchumi endelevu pamoja na huduma za kifedha.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Kilolo Bw. Reginard Mkemangwa amesema zaidi ya wagombea watano wametia nia ya kugombea jimbo la kilolo kupitia CHADEMA ambapo June 25 ni mwisho wa kurudisha fomu kwa wagombea.