Wednesday , 30th Nov , 2016

Kijiji cha Zepisa, kata ya Hombolo Bwawani Manispaa ya Dodoma, kinakabiliwa na tatizo la huduma za matibabu kwa kukosa zahanati kwa muda mrefu hali inayosababisha baadhi ya wajawazito kujifungulia porini pale wanapofuata zahanati vijiji vya jirani.

Maeneo ya Nguji Dodoma

Baadhi ya wananchi wa kijiji hicho kilichopo umbali wa zaidi ya kilomita 50 kutoka Manispaa ya Dodoma, wamesema miongoni mwa mama wajawazito wamekuwa wakijifungulia porini kutokana umbali wa kuifuata zahanati ya kata iliyopo umbali wa kilomita 13.

Mkunga wa jadi katika eneo hilo Bi. Evelini Lugolein mwenye miaka 80, amesema amefanya kazi ya kuzalisha wanawake wa kijiji hicho kwa muda mrefu na kuzalisha zaidi ya wajawazito 800 kutokana na kijiji hicho kukosa zahanati.

Kaimu Afisa mtendaji wa kata ya hombolo bwawani, daudi kamunya, amesema kijiji hicho ina changamoto kubwa ya huduma ya afya licha ya kuwa na kaya elfu moja mia mbili na ishiriki na nne wakazi zaidi ya elfu nne, lakini pamoja na kupigania kupata zahanati hakuna kilichofanyika.

Godwin Kunambi

Hata hivyo, Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma, Godwin Kunambi, amesema suala hilo kwa wanakijiji hao linashughulikiwa na manispaa yake.

Msikilize hapa Daudi Kamunya…Kaimu Afisa Mtendaji wa Kata