Monday , 25th Jul , 2016

Waumini wa Dini ya Kiislam wametakiwa kutumia vyema fursa ya Ibada ya Hija kwa ajili ya kujiimairisha kiroho na kujiandaa kuwa raia wema wa taifa la Tanzania.

Shekhe Mkuu wa Tanzania ambaye pia ni Mufti wa Tanzania, Aboubakar Zubeir Bin Ally.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI),Mhe. Suleiman Jaffo, wakati akizindua kitengo cha Hijja chini ya baraza kuu la waislam nchini Tanzania (Bakwata).

Mhe. Jaffo amesema kuwa kuanzisha kitwengo hicho kitapunguza utapeli uliokuwa unafanywa na baadhi ya watu kwa kudai kuwapeleka hija na hatimae kutokomea kusikojulikana.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa kitengo hicho cha Hijja kutoka BAKWATA, amesema kuwa ili kufanikisha Waislam wengi kutimiza ibada hiyo ya Hijja wamepunguza gharama za Kusafiri kutoka dola 5000 mpaka kufikia dola 3800 tu.

Sauti ya Naibu Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI),Mhe. Suleiman Jaffo.