Friday , 12th Feb , 2016

Viongozi wa Kiislamu nchini Uganda wamepinga wazo la mgombea urais Amama Mbabazi la kutaka kurejesha mwili wa aliyekuwa rais wa nchi hiyo Idd Amin.

Viongozi hao wamesema dini ya kiislamu haikubali mwili wa mtu kufukuliwa na kuzikwa tena huku wakisisitiza hatua ya Bw Amin kuzikwa Mecca ni hadhi kubwa katika Uislamu.

Msemaji wa Baraza Kuu la Waislamu Uganda Hajj Nsereko Mutumba amesema kuwa haamini kama Bw Mbabazi alikuwa na nia ya dhati alipotoa kauli hiyo.

Bw Mbabazi, aliyekuwa waziri mkuu kati ya 2011-2014, ni miongoni mwa wagombea saba wanaojaribu kufikisha kikomo uongozi wa miaka 30 wa Rais Yoweri Museveni.