
Hayo yamesemwa bungeni na Waziri Hussein Mwinyi wakati akijibu maswali ya wabunge kuhusu wizara yake juu ya utaratibu unaotumika kusajili vijana wanaojiunga JKT.
Akijibu swali hilo Waziri amesema kwamba kuna utaratibu wa kujitolea kwa wahitimu wa darasa la saba hadi chuo kikuu ambapo kwa mara hoja huingia vijana 5000 hadi 7000.
Kwa upande wa wanaohitimu kidato cha sita Waziri amesema ni sheria wote wahudhurie mafunzo hayo ila kutokana na upungufu wa kambi inabidi waende pungufu ambapo kwa msimu huu waliohitimu kidato cha sita 14000 wameshatangaziwa kujiunga kambini kuanza mafunzo.
Aidha Waziri amesisitiza kwamba serikali inaendelea na jitihada za kujenga vyumba katika makambi yaliyopo nchini ili yaweze kubeba wanafunzi wengi watakaohitimu kidato cha sita kwa pamoja kuliko ilivyo sasa.