Monday , 4th Apr , 2016

Zaidi ya Hekta 700 za misitu katika eneo la Chindi, wilaya ya Momba, Mkoa mpya wa Songwe, zimeharibiwa na wananchi wasiojulikana kwa kufanya shughuli za kibanadamu na kusababisha uharibifu wa mazingira.

Mkuu wa wilaya ya Momba, Richard Mbeho

Akizungumza katika misitu hiyo iliyofanyiwa uharibifu Mkuu wa wilaya ya Momba, Richard Mbeho amezitaka mamlaka husika ikiwemo jeshi la Polisi kuwatafuta viongozi wote wa vijiji vinavyozunguka misitu hiyo.

Bw. Mbeho amesema kuwa viongozi hao wanahusika na uvamizi wa misitu hiyo kutokana na kutoa vibali kinyume cha taratibu ya uvunaji wa miti hali inayosababisha uharibifu mkubwa.

Mkuu huyo wa wilaya amesema jambo la kwanza watamhoji afisa mtendaji wa kijiji cha Chindi ambae kwa maelezo yake inaoyesha kuwafahamu viongozi wanaowapeleka watu hao wanaofanya uvunaji wa misitu hiyo kwa kufanya shughuli za kuchoma mkaa na kupasua magogo.

Baadhi ya wanakijiji cha kijiji hicho cha Chindi wamesema wamesikitishwa na kitendo hicho cha uharibufu wa mazingiria hali inayopelekea ukosefu wa mvua za kutosha na kupelekea mazao yao kukauka mashambani na kusema ni vyema wanaofanya uharibifu huo kuchukuliwa hatua kali za kisheria.

Sauti yaMkuu wa wilaya ya Momba, Richard Mbeho akitoa maagizo ya kukamatwa walioharibu misitu