Wednesday , 14th May , 2014

Shirika linalojishughulisha na utetezi wa watu wenye ulemavu wa ngozi la Under the same Sun nchini Tanzania, limeitaka serikali kuzuia mara moja utoaji wa vibali kwa waganga wa kienyeji ambao baadhi yao huchangia mauaji ya watu wenye "albinism"

Mkurugenzi wa shirika la Under the Same Sun tawi la Tanzania, Bi. Vicky Ntetema, akiwa amekumbatiana na mmoja wa walemavu wa ngozi kuonyesha upendo alioano kwa jamii ya watu hao.

Mkurugenzi wa Under the Same Sun Bi. Vicky Ntetema ametoa kauli hiyo leo jijini Dar-es-Salaam wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kufuatia kuuwawa kwa Mungu Lugata, kijana mwenye albinism
usiku wa kumamkia tarehe 12 ya mwezi huu katika kijiji cha Gasuma huko Bariadi mkoani Simiyu.

Bi.Vicky amesema takwimu za mauaji wenye albinism zinaonesha kwamba mpaka sasa watu 73 wamekwishauawa tangu mwaka 2000 huku 49 wakinusurika kuuawa kutokana na imani za kishirikina.