Friday , 30th Jan , 2015

Hatimaye wafuasi 29 kati ya 30 wa chama cha wananchi (CUF) akiwemo Naibu Mkurugenzi wa Oganaizesheni, Uchaguzi na Bunge Shaweji Mketo na Naibu Mkurugenzi wa mawasiliano Abdul Kambaya wamepatiwa dhamana.

Licha ya wafuasi hao kupatiwa dhamana, mmoja ya watuhumiwa hao ambaye ni mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Sandali Bw Abdina Ali Abdina amelazimika kutolewa nje ya chumba cha mahakama baada ya kupata shinikizo la damu kutokana na mdhamini wake kuchelewa kukamilisha taratibu za dhamana.

Shauri hilo lipo mbele ya hakimu Emilius Mchauro wa mahakama ya hakimu mkazi kisutu, jijini Dar es Salaam ambapo wakili wa serikali   Hellen Mushi ambapo kwa upande wa wakili wanaowatetea  washitakiwa hao walianza kuwaongoza washtakiwa hao katika uwasilishwaji wa barua za dhamana na ndipo hakimu alipoanza kuwahoji wadhamini wawatuhumiwa.
 
Zoezi la kuwahoji wadhamini wa watuhumiwa lilipofika kwa mtu wa sita ndipo Bw Abdina Ali Abdina aliposhuhudua mdhamni wake akiwa kasimama bila ya barua mkononi.
 
Baada ya kukamilika kwa taratibu za kidhamana wanachama hao walikuwa rumande waliruhusiwa na furaha ilitanda katika viwanja vya mahakama hiyo.
 
Akizungumza mahakamani hapo naibu katibu mkuu wa chama hicho Mh Magdalena Sakaya amesema wapo bado wanaendelea kuhakisha kuwa wanachama wao wanakuwa huru na jambo kubwa wanaamni ipo siku haki itapatikana.
 
Itakumbukwa kuwa watuhumiwa hao walifikishwa mahakamani hapo Jan 29 mwaka huu wakikabiliwa na mashtaka matatu ikiwemo kufanya mkusanyiko tarehe 27 mwaka huu wenye nia ya kufanya maandamano kuelekea viwanja vya Zakhiem, Mbagala, Dar es Salaam bila ya kuwa na kibali .

Shauri hilo litatajwa tena Feb 12.