Mtendaji Mkuu OSHA, Dk. Akwilina Kayumba
Akizungumza jana na Waandishi wa habari nje ya mkutano wa pili wa baraza la wafanyakazi wa Osha,Mtendaji Mkuu wa OSHA, Dkt. Akwilina Kayumba amesema wafanyakazi hao walibainika kuwa na matizo ya kiafya ikiwemo kujaa vumbi katika mapafu, masikio kutosikia na matatizo mengine madogo madogo.
Dkt. Kayumba amesema kuwa madhara mengi yanawakuta wafanyakazi hasa wa viwandani ni kutokana na ukosefu wa elimu, hivyo wanakumbana na changamoto ya kuweza kujikinga ili wasiweze kupata matatizo ya Kiafya.
Kwa upande wa Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu, kazi ,vijana, ajira, na wenye Ulemavu, Anthony Mavunde, amewataka wafanyakazi wa wakala huyo kufaya kazi kwa kufuata sheria na kanuni zinazowaongoza.
Naye Mwakalishi wa Baraza Kuu la watumishi serikalini Ufedilis Athuman ametoa ushauri kwa serikali ni kuhakikisha maombo yanapelekwa na wakala huyo wa Usalama mahali pa kazi waweze kuyashughulikia haraka ili kuondoa changamoto hizo.