Friday , 24th Oct , 2014

Watu wasiofahamika wanaosadikiwa kuwa ni Mjambazi jana walivamia Benki ya Stanbic katika tawi la Mayfair jijini Dar es Salaam nchini Tanzania na kupora kiasi cha fedha ambacho kiasi chake bado hakijafahamika.

Kamanda kanda maalumu Dar es Salaam Kamishna Suleimani Kova

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa wa jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova ameziagiza benki zote za jijini humo kuhakikisha zinalindwa na askari polisi ili kukabiliana na uhalifu unaojitokeza mara kwa mara.

Kamanda Kova pia amesema wizi huo unaonekana ni mpango uliofanywa na baadhi ya watumishi wa banki hiyo kutokana na wezi hao kufanya tukio hilo na kuchukua fedha kwa urahisi Zaidi.

Aidha ameongeza kuwa waajiriwa wa mabenki hayo watafanyiwa uchunguzi pamoja na kuchukuliwa alama muhimu ikiwamo alama za vidole ili kukabiliana na uhalifu unaofanywa na baadhi ya watumishi wasiokuwa waaminifu.

Kova amesema kuwa katika uchunguzi wa awali wamegundua wizi wa mtandao wa ndani ya banki kwa sababu hakuna nguvu iliyotumika na wakapata taarifa kuwa, kuna watu wamefungiwa chooni lakini kuna vitufe vya kubonyeza vya hatari ili kutoa taarifa lakini havikubonyezwa.